Luke 20:41-44

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)

41 a bKisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi?
42 dDaudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi:

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
43 e hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
44 Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”

Copyright information for SwhNEN